Posts

62. BWANA WA MABWANA

BWANA WA MABWANA 1.    Bwana wa mabwana, Mwenye nguvu sana Twakusihi: Neno la milele Na liende mbele, Waongoke tele Kwa Mwokozi.   2.    Tunaowaona Wanavyopatana, Kulipinga, Hawataliweza Neno, kulitweza: Huwaje! Kucheza: Na upanga?   3.    Heri wajitunze Ili wapatane, Na Mwokozi; Watafute sana, Wapate kuona, Yesu kuwa Bwana, Mkombozi.   4.    Mungu awaita Wasije kukuta Pigo lake; Hakuona vyema Wakose uzima, Awape rehema, Waokoke.   5.    Mwenye utukufu Tunamshukuru Yeye pweke! Nasifiwe sana, Baba, naye Mwana, Na wa tatu tena Roho yake.

63. NDUGU WA KIROHONI

NDUGU WA KIROHONI 1.    Ndugu wa kirohoni Mliokombolewa, Tafakarini sana Yatupasayo.   Chorus: Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.   2.    Siku itatimia Tutakapoulizwa Wale wa nyumba zetu Na majirani.   3.    Tujitoeni, ndugu, Tukahubiri Injili. Atutumie Roho kuponya wengi.   4.    Wasiokombolewa Ni wengi vijijini, Wataokolewaje Tukiogopa?   5.    Bwana alijitoa Akapotewa mengi, Ili atuokoe, Tusiwe waoga.   6.    Aliyetununua, Kwa kuimwaga damu, Angalieni sana Msimwepuke.

64. UJARIBIWAPO, SIFANYE DHAMBI

UJARIBIWAPO, SIFANYE DHAMBI 1.    Ujaribiwapo, sifanye dhambi, Bali uzishinde, kwa Yesu kutii. Fuliza kiume ushinde tamaa; Yesu ni Mwokozi, hukuokoa. Chorus:   Umwombapo yu papo Akuongeze nguvu, Atakusaidia; Yesu atakufaa.   2.    Wepushe waovu, matusi dharau; Heshima la Mungu, kamwe sisahau; Fanya uhodari, uwe mpole, Atakuokoa hata milele.   3.    Avumiliaye hupewa taji; Tujaposumbuka tu washindaji, Na mwokozi wetu hutuwezesha Tusiwe kushindwa kama twakesha.

65. KATIKA SAFARI YETU

KATIKA SAFARI YETU 1.    Katika safari yetu Kwenda Mbinguni Tusiishe siku zetu Usingizini. Chorus: Ng’oani! Tujifungeni, Twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; Tusihofu tu.   2.    Atwekwe badala yetu, Mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu Atapokea.   3.    Kisimani, maji tele, Maji mazima! Maji hayo, Ya milele Yana neema.   4.    Njiani miiba mingi, Yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, Sana zakaza.   5.    Kweli, njia ya Mbinguni Ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, Mara hufika.

66. PO POTE MASHAMBA YAJAA

PO POTE MASHAMBA YAJAA 1.    Po pote mashamba yajaa, Tele nafaka pevu, Po pote yang’aa meupe Bondeni na nyandani.   Chorus: Mwenye mavuno, twasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe.   2.    Wapeleke uchaoni, Waende na jotoni, Mpaka jua lishukapo Wakusanye ko kote.   3.    Watenda kazi wa Bwana, Mlete sasa mazao, Na jioni ingieni Kwake na furaha kuu.

67. BWANA ULIYEWAITA

  BWANA ULIYEWAITA 1.    Bwana uliyewaita Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; Wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa.   2.    Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? “Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana.”   3.    Nitume na mimi, Bwana Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia.   4.    Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini Wewe waweza Kutufanya tayari. Neno lako tulijue, Tupe na roho yako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako.

68. MUNGU MSAADA WETU

MUNGU MSAADA WETU 1.    Mungu msaada wetu Tangu miaka yote, Ndiwe tumaini letu La zamani zote.   2.    Kivuli cha kiti chako Ndiyo ngome yetu. Watosha mkono wako Ni ulinzi wetu.   3.    Kwanza havijakuwako Nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako Twakaa salama.   4.    Na miaka elfu ni kama Siku moja kwako; Utatulinda daima Tu wenyeji wako.   5.    Binadamu huondoka, Mwisho hana kitu; Kama ndoto hutoweka Ndivyo hali yetu.   6.   Ila Wewe Mungu wetu Ndiwe wa kudumu; Ndiwe bora, Ngome yetu Twakaa dawamu.