Posts

Showing posts from March, 2022

62. BWANA WA MABWANA

BWANA WA MABWANA 1.    Bwana wa mabwana, Mwenye nguvu sana Twakusihi: Neno la milele Na liende mbele, Waongoke tele Kwa Mwokozi.   2.    Tunaowaona Wanavyopatana, Kulipinga, Hawataliweza Neno, kulitweza: Huwaje! Kucheza: Na upanga?   3.    Heri wajitunze Ili wapatane, Na Mwokozi; Watafute sana, Wapate kuona, Yesu kuwa Bwana, Mkombozi.   4.    Mungu awaita Wasije kukuta Pigo lake; Hakuona vyema Wakose uzima, Awape rehema, Waokoke.   5.    Mwenye utukufu Tunamshukuru Yeye pweke! Nasifiwe sana, Baba, naye Mwana, Na wa tatu tena Roho yake.

63. NDUGU WA KIROHONI

NDUGU WA KIROHONI 1.    Ndugu wa kirohoni Mliokombolewa, Tafakarini sana Yatupasayo.   Chorus: Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.   2.    Siku itatimia Tutakapoulizwa Wale wa nyumba zetu Na majirani.   3.    Tujitoeni, ndugu, Tukahubiri Injili. Atutumie Roho kuponya wengi.   4.    Wasiokombolewa Ni wengi vijijini, Wataokolewaje Tukiogopa?   5.    Bwana alijitoa Akapotewa mengi, Ili atuokoe, Tusiwe waoga.   6.    Aliyetununua, Kwa kuimwaga damu, Angalieni sana Msimwepuke.

64. UJARIBIWAPO, SIFANYE DHAMBI

UJARIBIWAPO, SIFANYE DHAMBI 1.    Ujaribiwapo, sifanye dhambi, Bali uzishinde, kwa Yesu kutii. Fuliza kiume ushinde tamaa; Yesu ni Mwokozi, hukuokoa. Chorus:   Umwombapo yu papo Akuongeze nguvu, Atakusaidia; Yesu atakufaa.   2.    Wepushe waovu, matusi dharau; Heshima la Mungu, kamwe sisahau; Fanya uhodari, uwe mpole, Atakuokoa hata milele.   3.    Avumiliaye hupewa taji; Tujaposumbuka tu washindaji, Na mwokozi wetu hutuwezesha Tusiwe kushindwa kama twakesha.

65. KATIKA SAFARI YETU

KATIKA SAFARI YETU 1.    Katika safari yetu Kwenda Mbinguni Tusiishe siku zetu Usingizini. Chorus: Ng’oani! Tujifungeni, Twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; Tusihofu tu.   2.    Atwekwe badala yetu, Mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu Atapokea.   3.    Kisimani, maji tele, Maji mazima! Maji hayo, Ya milele Yana neema.   4.    Njiani miiba mingi, Yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, Sana zakaza.   5.    Kweli, njia ya Mbinguni Ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, Mara hufika.

66. PO POTE MASHAMBA YAJAA

PO POTE MASHAMBA YAJAA 1.    Po pote mashamba yajaa, Tele nafaka pevu, Po pote yang’aa meupe Bondeni na nyandani.   Chorus: Mwenye mavuno, twasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe.   2.    Wapeleke uchaoni, Waende na jotoni, Mpaka jua lishukapo Wakusanye ko kote.   3.    Watenda kazi wa Bwana, Mlete sasa mazao, Na jioni ingieni Kwake na furaha kuu.

67. BWANA ULIYEWAITA

  BWANA ULIYEWAITA 1.    Bwana uliyewaita Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; Wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa.   2.    Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? “Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana.”   3.    Nitume na mimi, Bwana Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia.   4.    Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini Wewe waweza Kutufanya tayari. Neno lako tulijue, Tupe na roho yako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako.

68. MUNGU MSAADA WETU

MUNGU MSAADA WETU 1.    Mungu msaada wetu Tangu miaka yote, Ndiwe tumaini letu La zamani zote.   2.    Kivuli cha kiti chako Ndiyo ngome yetu. Watosha mkono wako Ni ulinzi wetu.   3.    Kwanza havijakuwako Nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako Twakaa salama.   4.    Na miaka elfu ni kama Siku moja kwako; Utatulinda daima Tu wenyeji wako.   5.    Binadamu huondoka, Mwisho hana kitu; Kama ndoto hutoweka Ndivyo hali yetu.   6.   Ila Wewe Mungu wetu Ndiwe wa kudumu; Ndiwe bora, Ngome yetu Twakaa dawamu.

69. TWENDENI ASKARI

TWENDENI ASKARI 1.    Twendeni askari, watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, tumwandame juu. Ametangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini. Chorus: Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.   2.    Jeshi la Shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia, Kelele za shangwe zivume nchini; Ndugu inueni zenu sauti.   3.    Kweli kundi dogo, watu wa Mungu Sisi na mababa tu moja fungu. Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini moja, na moja dini.   4.    Haya mbele watu nasi njiani, Inueni myoyo, nanyi sifuni; Heshima na sifa ni ya Mfalme, Juu hata chini, sana zivume.

70. YESU ATUCHUNGA

YESU ATUCHUNGA 1.    Yesu atuchunga, Mchunga wetu, Naye atufuta Machozi yetu; Mkononi mwake Hatuna hofu, Daima twapata Kwake wokovu.   2.    Yesu atuchunga Tumemjua, Na sauti yake Twaitambua; Naye akituonya Ni kwa upole, Tu kondoo zake Hata milele.   3.    Yesu atuchunga; Aliwafia Kondoo wakubwa Na wana pia; Kwamba awajua, Kondoo zake, Hutiwa alama Ya damu yake.   4.    Yesu atuchunga; Mikono yake Imewaambata Kondoo zake; Hapati wadhuru Adui yule, Yesu awalinda.

71. MTETEENI YESU

MTETEENI YESU 1.    Mteteeni Yesu, Mlio askari; Inueni beramu, Mukae tayari, Kwenda nae vitani, Sisi hatuchoki Hata washindwe pia Yeye amiliki.   2.    Mteteeni Yesu, Vita ni vikali; Leo siku ya Bwana, Atashinda kweli, Waume twende naye, Adui ni wengi, Lakini kwake Bwana Tuna nguvu nyingi.   3.    Mteteeni Yesu, Wenye ushujaa; Nguvu zenu za mwili Hazitatufaa; Silaha ya injili Vaeni daima, Kesheni mkiomba, Sirudini nyuma.   4.    Mteteeni Yesu, Vita ni vikali, Wengi wamdharau, Hawamkubali, Ila atamiliki Tusitie shaka, Kuwa naye vitani Twashinda hakika.

72. TWENDENI! HARAKA!

TWENDENI! HARAKA! 1.    Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza. Bwana alisema nendeni po pote Kawafundisheni mataifa yote. Pelekeni Injili kwa Jina la Yesu. Upesi! Twendeni haraka!   2.    Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La upendo wa Mungu kwa watu wote; Aliyeupenda sana ulimwengu Akamtoa Yesu Mwana wake pekee Kaleta wokovu, tumtangazeni. Upesi! Twendeni haraka!   3.    Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La uzima kwa watu waliokufa. Mateka ya Shetani litafungua Litaponyesha na kuwapa amani. Twendeni upesi, tukawaokoe. Upesi! Twendeni haraka!

73. YESU ZAMANI BETHILEHEMU

YESU ZAMANI BETHILEHEMU 1.    Yesu zamani Bethilehemu, Aliyezaliwa kwa aibu, Ndiye mwakozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi.   Chorus: Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi; Ndiye mwaokozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi.   2.    Yesu akafa msalabani, Kuniponya akalipa deni, Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi! Chorus:   Kunifia mimi! Kunifia mimi! Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi.   3.    Ni Yeye huyo tangu asili; Na nilipotanga-tanga mbali Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi.   Chorus: Kuniita mimi; Kuniita mimi; Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi. 4.    Yesu kristo atarudi tena, Hilo lanifurahisha sana. Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi.   Chorus: Kunijia mimi, kunijia mimi, Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi.

74. WACHUNGA WALIPOLINDA

WACHUNGA WALIPOLINDA 1.    Wachunga walipolinda Kucha nyama zao, Malaika mtukufu Alishuka kwao.   2.    Wakacha sana wachunga, Akawatuliza, “Nawaletea habari Ya kuwapendeza.”   3.    “Mji ule wa Daudi Leo amezawa Mwokozi ni Kristo Bwana, Ilivyoandikwa”.   4.    “Huyo mwana wa Mbinguni Ataonekana, Amelazwa kihorini Malazi hapana.”   5.    Alipokwisha yanena Malaika hao Waliimba wimbo huu Usio na mwisho:   6.    “Enzi ni yake Munju juu, Na nchi salama, Kwa watu nao radhi kuu, Sasa na daima.”

75. WAIMBA SIKIZENI

WAIMBA SIKIZENI 1.    Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni; Wimbo wa tamu sana Wa pendo zake Bwana, “Duniani salama, Kwa wakosa rehema.” Sisi sote na twimbe Nao wale wajumbe; Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.   2.    Ndiye Bwana wa Mbingu, Tangu milele Mungu, Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali; Ametoka enzini Kuja ulimwenguni Mwokozi atufie, Ili tusipotee. Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.   3.    Mtukufu wa amani Ametoka Mbinguni, Jua la haki, ndiye Atumulikiaye; Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi, Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya, Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.   4.    Njoo upesi, Bwana, Twakutamani sana; Kaa nasi, mwokozi Vita hatuviwezi; Vunja kichwa cha nyoka, Sura zako andika, Tufanane na Wewe, Kwetu sifa upewe, Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.

76. NJONI NA FURAHA

NJONI NA FURAHA 1.    Njoni na furaha, enyi wa imani, Njoni Bethilehemu upesi ! Amezaliwa jumbe wa Mbinguni; Njoni tumuabudu, njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.   2.    Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga, Amekuwa radhi kuzaliwa; Mungu wa kweli, wala si kiumbe; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.   3.    Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu, Mbingu zote na zijae sifa; Sifuni Mungu aliye Mbinguni; Njoni tumuabudu, njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.   4.    Ewe Bwana mwema, twakubarikia, Yesu, utukufu uwe wako; Neno la Baba limekuwa mwili; Njoni tumuabudu, njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.

77. MSALABANI PA MWOKOZI

MSALABANI PA MWOKOZI 1.    Msalabani pa mwokozi, Hapo niliomba upozi, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu. Chorus: Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa Mpenzi, Mwana wa Mungu.   2.    Chini ya mti msumbufu, Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu. Chorus:   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.   3.    Aliniokoa dhambini, Ikawa kunikaa ndani, Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu.   Chorus: Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu.   4.    Damu ya Yesu ya thamani, Huniokoa makosani, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu. Chorus:   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.   5.    Hicho kijito cha gharama, Leo jivike kwa kuzama, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu. Chorus:   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.

78. SIOSHWI DHAMBI ZANGU

SIOSHWI DHAMBI ZANGU   1.    Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hapendezewi Mungu, Bila damu yake Yesu. Chorus: Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.   2.    La kunisafi sina Ila damu yake Yesu. Wala udhuru tena, Ila damu yake Yesu.   3.    Sipati patanishwa, Bila damu yake Yesu. Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu.   4.    Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu. Wema wala amani, Bila damu yake Yesu.   5.    Yashinda ulimwengu, Hiyo damu yake Yesu. Na kutufikisha juu, Hiyo damu yake Yesu.   6.    Twaimba: Utukufu Una damu yake Yesu. Milele twaisifu, Hiyo damu yake Yesu.

79. MSALABA WA AIBU

MSALABA WA AIBU   1.    Msalaba wa aibu, Ulinipa amani; Uliniondoa kifungoni, Nilimotesekea.   2.    Ee, Mwokozi wangu, Yesu Nitamwendea nani? Najiweka msalabani, Nikaoshwe damuni.   3.    Nakupenda Bwana Yesu, Kwa kunipenda kwako, Napendezwa nikutumikie Maisha yangu yote.   4.    Usifiwe Bwana Yesu, Kwa ulivyonifia, Aleluya, nakushukuru, Uliyenikomboa.   5.    Msalaba ulishinda Nguvu zake adui, Ili mimi nikombolewe, Niwe mwana wa Mungu.

80. WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA

WAMWENDEA YESU KWA KUSAFIWA 1.    Wamwendea Yesu kwa kusafiwa, Na kuoshwa kwa damu ya kondoo? Je neema yake umemwagiwa, Umeoshwa kwa damu ya kondoo? Chorus: Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo?   2.      Wamwandama daima Mkombozi Na kuoshwa kwa damu ya kondoo? Yako kwa Msulubiwa makazi, Umeoshwa kwa damu ya kondoo?   3.    Atakapokuja Bwana – arusi Uwe safi kwa damu ya kondoo! Yafae kwenda mbinguni mavazi Yafuliwe kwa damu ya kondoo.   4.    Yatupwe yalipo na takataka, Na uoshwe kwa damu ya kondoo. Huoni kijito chatiririka Na uoshwe kwa damu ya kondoo?

81. CHINI YA MSALABA

CHINI YA MSALABA 1.    Chini ya Msalaba Nataka simama; Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema; Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.   2.    Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili; Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli; Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani, Msalaba umekuwa Ngazi ya Mbinguni.   3.    Na Yesu Msalabani Walimkemea, Alikufa niokoke Niliyepotea; Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda, Nisiyestahili.   4.    Atakayeonana, Na Yesu Mbinguni, Njia yake aanzapo Ni Msalabani; Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana, Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.

82. SIONI HAYA KWA BWANA

SIONI HAYA KWA BWANA 1.    Sioni haya kwa Bwana Kwake nitang’ara! Mti wake sitakana, Ni neno imara! Chorus:   Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo; Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo.   2.    Kama kiti chake vivyo Ni yake ahadi, Alivyowekewa navyo Kamwe havirudi.   3.    Bwana wangu, tena Mungu Ndilo lake jina! Hataacha roho yangu Wala kunikana.   4.    Atakiri langu jina, Mbele za Babaye, Anipe pahali tena Mbinguni nikae.

83. KWA WINGI WA NYAMA

  KWA WINGI WA NYAMA 1.    Kwa wingi wa nyama, Na sadaka pia, Hupata wapi salama, Kwondoa hatia?   2.    Sadaka ni Yesu, Hwondoa makosa; Dhabihu mwenye jina kuu, Atanitakasa.   3.    Kwa yangu imani, Nikuweke sasa Mkono mwako kichwani Kukiri makosa.   4.    Roho yakumbuka Mambo ya Mtini, Mzigo ulijitweka, Ndiyo yangu deni.   5.    Deni hutanguka, Tukimuamini; Kwa damu tumeokoka, Twimbe furahani.

84. NIWONAPO MTI BORA

NIWONAPO MTI BORA 1.    Niwonapo Mti bora Kristo aliponifia Kwangu pato ni hasara Kiburi nakichukia.   2.    Na nisijivune, Bwana Ila kwa mauti yako; Upuzi sitaki tena, Ni chini ya damu yako.   3.    Tangu kichwa hata nyayo, Zamwagwa pendo na hamu, Ndako pweke hamu hiyo, Pendo zako zimetimia.   4.    Vitu vyote vya dunia, Si sadaka ya kutosha; Pendo zako zaniwia Nafsi, mali, na maisha.

85. NI "MTU WA SIMANZI"

NI "MTU WA SIMANZI" 1.    Ni “Mtu wa Simanzi”, Mwana wa mwenye enzi Mwenye mengi mapenzi! Asifiwe Bwana Yesu!   2.    Akawa matesoni, “Mungu mwana" yakini Akatoka Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!   3.    Akapata dhihaka, Mzoea – mashaka Ndiye yetu sadaka: Asifiwe Bwana Yesu!   4.    Tu wenye dhambi sana; Kwake dhambi hamna, Na Mungu twapatana: Asifiwe Bwana Yesu!   5.    Alikufa mtini, Akalia dhikini, Sasa yuko Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!   6.    Punde atarejea, Yesu kutunyakua, Ndipo tutamwimbia: Asifiwe Bwana Yesu!