85. NI "MTU WA SIMANZI"

NI "MTU WA SIMANZI"

1.  Ni “Mtu wa Simanzi”,
Mwana wa mwenye enzi
Mwenye mengi mapenzi!
Asifiwe Bwana Yesu!
 
2.  Akawa matesoni,
“Mungu mwana" yakini
Akatoka Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!
 
3.  Akapata dhihaka,
Mzoea – mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Asifiwe Bwana Yesu!
 
4.  Tu wenye dhambi sana;
Kwake dhambi hamna,
Na Mungu twapatana:
Asifiwe Bwana Yesu!
 
5.  Alikufa mtini,
Akalia dhikini,
Sasa yuko Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!
 
6.  Punde atarejea,
Yesu kutunyakua,
Ndipo tutamwimbia:
Asifiwe Bwana Yesu!

Comments

Popular posts from this blog

67. BWANA ULIYEWAITA

68. MUNGU MSAADA WETU

81. CHINI YA MSALABA