81. CHINI YA MSALABA

CHINI YA MSALABA

1.  Chini ya Msalaba
Nataka simama;
Ndio mwamba safarini,
Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu
Ni tuo kamili,
Tatua mzigo wangu
Wakati wa hari.
 
2.  Hapa ni pema sana,
Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana,
Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa
Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa
Ngazi ya Mbinguni.
 
3.  Na Yesu Msalabani
Walimkemea,
Alikufa niokoke
Niliyepotea;
Naona ajabu sana
Ya mambo mawili
Jinsi alivyonipenda,
Nisiyestahili.
 
4.  Atakayeonana,
Na Yesu Mbinguni,
Njia yake aanzapo
Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu,
Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu
Pamoja na Bwana.

Comments

Popular posts from this blog

67. BWANA ULIYEWAITA

68. MUNGU MSAADA WETU